Soka Safi
Tuesday, January 5, 2021
NAMUNGO YAFANYA KWELI KOMBE LA SHIRIKISHO BARANI AFRIKA
Klabu ya Namungo FC imefanikiwa kutinga hatua ya 32 bora ya mashindano ya shirikisho barani Afrika hii ni baada ya kuwalazimisha sare ya 3 - 3 El Hilal Obeid iliyokuwa nyumbani huko Sudan. Magoli ya Namungo FC yalifungwa na Stephen Sey dakika ya 2', Bigirimana Blaise dakika ya 38', Edward Manyama dakika ya 49' kwa matokeo haya aggregate ilisoma Namungo FC 5 - 3 El Hilal Obeid baada ya Namungo kuibuka na ushindi mechi ya nyumbani iliyochezwa chamazi kwa magoli 2 - 0. Hivyo Namungo inasubiri timu nyingine 16 zitakazotolewa kwenye Champions League kwenye raundi ya kwanza kwa ajili ya kucheza nazo na kama itafanikiwa kupita itaingia hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika . Kila la heri Namungo katika safari hii mliyoianza 🙏🙏
Friday, March 8, 2019
Hapa ndipo kichuya alipofeli
Naam! ni Shiza Ramadhan Kichuya.
Winga mzaliwa wa Morogoro mwenye uwezo wa kutumia mguu wake wa kushoto kiufasaha.
Winga mzaliwa wa Morogoro mwenye uwezo wa kutumia mguu wake wa kushoto kiufasaha.
Hapo kabla Tanzania haikumtambua mwanadamu huyu.
Hata baadhi ya viongozi wa Simba waliokuja kumsajili hawakuwahi kujua au hata kufikiri kama mji wa Morogoro kulikuwa na mchezaji aliyeitwa Shiza Kichuya.
Hata baadhi ya viongozi wa Simba waliokuja kumsajili hawakuwahi kujua au hata kufikiri kama mji wa Morogoro kulikuwa na mchezaji aliyeitwa Shiza Kichuya.
Ni skauti nzuri iliyofanywa na viongozi wa Mtibwa Sugar Fc ambao walifanikiwa kuigundua dhahabu iliyojifukia mavumbini, "Shiza Ramadhan Kichuya".
Alikuwa na wakati mzuri pale Mtibwa Sugar. Anakumbukwa vyema na mabeki waliowahi kukutana nae kwenye mechi za ligi kuu Tanzania bara na hata kwenye kombe la mapinduzi.
Hakika walipata wakati mgumu kuweza kumdhibiti.
Hakika walipata wakati mgumu kuweza kumdhibiti.
Kama ilivyo kawaida ya viongozi wa timu kubwa kutamani kila mchezaji bora awepo kwenye kikosi chao. Shiza Ramadhani Kichuya akasajiliwa na Simba.
Ulikuwa ni usajili bora pia, Kichuya alikuwa ni winga halisi.
Najaribu kuchambua kwenye makablasha yangu sikumbuki kama Simba ilipata winga mzuri baada ya kuondokewa na Uhuru Selemani, walihangaika sana kumpata winga halisi.
Shiza Kichuya akaja kuutibu ugonjwa wao.

Maisha ya mwanzoni pale Simba yalikuwa ni bora.
Aliimbwa kila kona, jezi namba 25 mgongoni.
Aliimbwa kila kona, jezi namba 25 mgongoni.
Hii iliwaamisha mashabiki wa Simba kuwa Kichuya ni mrithi sahihi wa Okwi.
Okwi yule wa miaka nane iliyopita sio huyu wa leo ambae yupo magharibi ya soka lake.
Okwi yule wa miaka nane iliyopita sio huyu wa leo ambae yupo magharibi ya soka lake.
Nani halikumbuki lile bao la kona ya maajabu? tena kwenye mechi ya Simba na Yanga wakati ambao Kichuya akiirudisha Simba mchezoni.
Bila shaka ni kumbukumbu nzuri itayokuwa ngumu kufutika kwake, hata leo nikirudi kwetu Kilwa bado wanalizungumzia bao lile.
Kichuya aliweza kuibeba Simba mgongoni mwake. Mara kadhaa aliweza kuamua kwenye mechi ngumu kwa kufunga au kutengeneza bao.
Hakika alikuwa ni mfalme asievikwa taji pale Simba.
Baada ya Kichuya kuiteka Tanzania taratibu akaanza kujisahau, akahisi ameshinda kila kitu.
Akawa hatishi tena, hata wale waliokuwa wakimuogopa wakaanza kumzoea.
Alikuwa kwenye usingizi wa pono.
Akawa hatishi tena, hata wale waliokuwa wakimuogopa wakaanza kumzoea.
Alikuwa kwenye usingizi wa pono.
Siku chache zilizopita Kichuya ameyaanza maisha yake mengine ya soka.
Amenunuliwa na timu ya Pharco Fc inayoshiriki ligi daraja la pili huko Misri na kutolewa kwa mkopo kwenye timu ya ENPPI Fc inayocheza ligi kuu.
Hii ni faida kwake na kwa taifa kwa ujumla.
Dua zangu zote kwake.

Hakuna aliejali sana usajili wake. Unajua kwanini? Thamani ya Kichuya ilishuka pale Simba. Alikuwa ni kama punje moja ya mchele kwenye kiroba cha kilogramu mia moja, hakuna ataejali kama itadondoka.
Wakati ambao Kichuya anaondoka Simba kuna sura mpya inayokuja vizuri.
Rashid Juma.
Kijana mwenye kipaji halisi cha soka.
Rashid Juma.
Kijana mwenye kipaji halisi cha soka.
Ninachojivunia niliwahi kumjua Rashid kabla ya watanzania walio wengi, unajua kwanini? Mara kadhaa nilikuwa nikimshuhudia akiitumikia timu ya mtaani kwetu Toangoma "kamuulizeni kama atabisha".
Kwa wakati huo ambao Rashid alikuwa akicheza mechi za makombe ya mbuzi hata wale wauzu kahawa waliuona uwezo wake.
Mijongeo yake,chenga za maudhi,uwezo mkubwa wa kukimbia na mpira na kufunga uliwafanya watu wazima wamshangilie kila anapokuwa na mpira.
Mijongeo yake,chenga za maudhi,uwezo mkubwa wa kukimbia na mpira na kufunga uliwafanya watu wazima wamshangilie kila anapokuwa na mpira.
Kwa sasa Rashid yupo Simba.
Aussems amejenga imani kwake. Mara kwa mara anampa nafasi ya kucheza na amekuwa hamuangushi kocha wake.
Namuona Kichuya mpya ndani yake, tena yule Kichuya aliekuwa bora zaidi.
Aussems amejenga imani kwake. Mara kwa mara anampa nafasi ya kucheza na amekuwa hamuangushi kocha wake.
Namuona Kichuya mpya ndani yake, tena yule Kichuya aliekuwa bora zaidi.
Mbali na hayo lazima Rashid ajue kuwa anacheza kwenye timu ya aina gani.
Kama ataacha kufanya bidii ya mazoezi na kubweteka basi ajue kuwa ni rahisi sana kwake kupotea.
Kama ataacha kufanya bidii ya mazoezi na kubweteka basi ajue kuwa ni rahisi sana kwake kupotea.
Kwa somo lenye uhai akipitia vizuri kitabu cha Kichuya aangalie wapi mwenzake alikosea "ili asije kupaka rangi gogo lililoliwa na mchwa".
Tamati.
Subscribe to:
Posts (Atom)