Tuesday, January 5, 2021
NAMUNGO YAFANYA KWELI KOMBE LA SHIRIKISHO BARANI AFRIKA
Klabu ya Namungo FC imefanikiwa kutinga hatua ya 32 bora ya mashindano ya shirikisho barani Afrika hii ni baada ya kuwalazimisha sare ya 3 - 3 El Hilal Obeid iliyokuwa nyumbani huko Sudan. Magoli ya Namungo FC yalifungwa na Stephen Sey dakika ya 2', Bigirimana Blaise dakika ya 38', Edward Manyama dakika ya 49' kwa matokeo haya aggregate ilisoma Namungo FC 5 - 3 El Hilal Obeid baada ya Namungo kuibuka na ushindi mechi ya nyumbani iliyochezwa chamazi kwa magoli 2 - 0. Hivyo Namungo inasubiri timu nyingine 16 zitakazotolewa kwenye Champions League kwenye raundi ya kwanza kwa ajili ya kucheza nazo na kama itafanikiwa kupita itaingia hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika . Kila la heri Namungo katika safari hii mliyoianza 🙏🙏
Subscribe to:
Posts (Atom)